Diamond Platnumz asaini dili nono la mamilioni, aungana na Rick Ross

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amelamba shavu nono la kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya vinywaji vikali ya Luc Belaire ya nchini Ufaransa.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kampuni hiyo imethibitisha kuwa Diamond Platnumz atakuwa mwanafamilia mpya kwenye kutangaza bidhaa zao za Belaire na kuungana na Mastaa kibao duniani ambao pia ni mabalozi wa bidhaa hiyo akiwemo Rick Ross.

Baada ya taarifa hizo rapa kutoka Marekani Rick Ross, nae pia alimkaribisha Diamond Platnumz  kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika ‘Self Made Tastes Better’ caption iliyoambana na picha ya Diamond Platnumz .

A post shared by The Boss Rick Ross,Yung Renzel (@richforever) on Sep 9, 2017 at 9:38am PDT

Dili hilo ambalo bado halijawekwa wazi ni kiasi gani Diamond Platnumz ataingiza baada ya kusaini na kampuni hiyo, lakini huenda likawa ni dili la mamilioni ya fedha kwani Rick Ross ambaye pia ni Balozi wa Belaire anakadiriwa kulipwa kiasi cha Dola milioni 4.1, zaidi ya Tsh bilioni 8.

Sharing is caring!